Wednesday, March 2, 2016

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, ATEMBELEA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WATENDAJI MGODI WA CHUMVI NYANZA.


Mkurugenzi wa Mgodi wa chumvi wa Nyanza (kulia), Mukesh Mamlani wa mgodi huo,  Bonny Mwaipopo (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani  wakati  alipokutana nao hivi karibuni katika ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amefanya mazungumzo na watendaji wa mgodi wa chumvi wa Nyanza uliopo mkoani Kigoma ambao walifika Wizara ya Nishati na Madini ili kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusu mgodi huo
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Katikati), Dkt. Medard Kalemani,  akizungumza  na  watendaji wa Mgodi wa Nyanza, Bonny Mwaipopo ( wa kwanza kushoto) na Mukesh Mamlani (wa pili kushoto) katika kikao kilichofanyika  hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini. Kulia ni Mjiolojia Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Aloyce Tesha.

Tuesday, March 1, 2016

KITENGO CHA USTAWI WA JAMII TANZANIA KIMELAANI VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA





AFISA USTAWI WA JAMII BW.SHIJA NUMBU
Kitengo cha ustawi wa jamii Tanzania kimelaani vitendo vya  unyanyasaji wa kijinsia vinavyofanyika na jamii mbalimbali hapa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Afisa ustawi wa jamii mkoani Arusha BW.SHIJA NUMBU wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa  jamii nyingi zinajihusisha na vitendo vya unyanyasaji hasa kwa watoto wa kike.
 
Afisa ustawi wa jamii mkoa wa arusha bw shija numbu akiongea na waandishi 


wa habari ofisini kwake
 Bw. shija amesema miongoni mwa vitendo hivyo ni
Ukeketaji,kuozeshwa kwa mtoto wa kike kwa lazima pamoja na ndoa za utotoni.
Hali hiyo inampelekea mtoto wa kike kukosa haki yake ya msingi kama vile Elimu,Malezi,Kusikilizwa,Kutoa maamuzi binafsi na kupoteza utu wa mtu.
Kadhalika ameitaka jamii kufahamu nafasi ya mtoto wa kike katika taifa  na kutambua kuwa ndoa ni maridhiano baina ya watu wawili hivyo utu wa mtu hauwezi kulinganishwa na hali ya maisha.
Kwa upande wake mkazi wa sanawari Bi Asha Juma ameiomba serikali kushirikiana na ustawi wa jamii kupitia mahakama kwa kuweka adhabu na ulinzi wa kutosha kwa jamii zinazohusika na vitendo hivyo.

Monday, February 29, 2016

Kaburi la pamoja lapatikana Burundi



Image copyrightReuters
Image captionUtawala wa mji mkuu wa Bujumbura Burundi wamegundua kaburi la halaiki linaloshukiwa kuwa na takriban miili 30.
Maafisa wa polisi na utawala wa mji mkuu wa Bujumbura Burundi wamegundua kaburi la pamoja linaloshukiwa kuwa na takriban miili 30.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Prime Ndikumagenge anasema kuwa miili 3 na fuvu la kichwa vilipatikana katika eneo la Mutakura Kaskazini mwa Bujumbura.
Kitongoji hicho cha Mutakura ni moja ya ile iliyosheheni wafuasi wa upinzani ambao walijitokeza mabarabarani wakiandamana kupinga kauli ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu uongozini.
Nkurunziza alitangaza nia ya kuwania muhula wa tatu mwezi Aprili mwaka uliopita kinyume cha katiba akidai kuwa mhula wa kwanza hakuchaguliwa na umma.
Image copyrightReuters
Image captionMeya huyo leo amekiri kuwa utawala wake ulizika miili ya watu 58 katika makaburi ya halaiki katika makaburi yanayofahamika.
Wapinzani wake hata hivyo wanadai kuwa alikiuka katiba ya taifa.
Meya wa mji wa Bujumbura Freddy Mbonimpa anasema walipokea habari hiyo kutoka kwa ''wahuni waliojisalimisha kwa utawala''.
Haikuelezwa kwa hakika waliuawa lini au na nani na nani aliyewazika pahala hapo.
Meya huyo hata hivyo alidai kuwa waliopatikana wameuawa walikuwa ni wafuasi wa rais Nkurunziza.
Image copyright
Image captionKaburi la halaiki lapatikana Burundi
Kuwepo kwa makaburi ya halaiki kuligunduliwa kwanza na kundi linalopigania haki za kibinadamu la Amnesty International mwezi Januari.
Ripoti hiyo ya kundi la kutetea haki za binadamu la lilichapishwa tarehe 11 Desemba mwaka uliopita siku moja baada ya serikali kukiri kuwa wamewaua watu 79 na kupoteza maafisa 8 wa polisi.
Meya huyo leo amekiri kuwa utawala wake ulizika miili ya watu 58 katika makaburi ya halaiki katika makaburi yanayofahamika.
Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa zaidi ya watu 430 waliuawa nchini Burundi tangu kauli ya rais Nkurunziza kubainika mwezi Aprili.

Kigogo wa Republican amkataa Trump


 
TrumpImage copyrightGetty
Image captionTrump ametuhumiwa kwa kuwagawanya Wamarekani
Seneta wa Nebraska Ben Sasse amesema hatamuunga mkono mgombea urais anayengoza miongoni mwa wagombea wa chama cha Republican Donald Trump.
Sasse ndiye mwachama wa kwanza wa ngazi ya juu wa chama cha Republican aliyechaguliwa kutangaza hadharani kwamba hatamuunga mkono Trump.
Amesema amesikitishwa sana na kuvunjwa moyo na mfanyabiashara huyo na kwamba atamtafuta mgombea mwingine wa kumuunga mkono iwapo Trump atashinda uteuzi wa Republican.
Bw Trump tayari ameshinda uchaguzi wa mchujo katika majimbo matatu kati ya manne yaliyofanya mchujo kufikia sasa.
Aidha, anaongoza kwenye kura za maoni katika majimbo 11 ambayo yatapiga kura ya mchujo Jumanne.
Uchaguzi wa leo wa mchujo ambao hufanya siku hii kujulikana kama “Jumanne Kuu” huwa muhimu sana kwa wagombea kwani huamua wale walio na nafasi ya kushinda na wale wasio na uwezekano wa kushinda.
"Iwapo Donald Trump atakuwa mgombea wa Republican, nitamtafuta mgombea mwingine, mhafidhina au anayetetea katiba,” Seneta Sasse amesema kwenye ujumbe aliopakia katika ukurasa wake wa Facebook.
"Bw Trump ameangazia sana kuwagawanya Wamarekani, na kubomoa badala ya kujenga taifa hili tukufu,” ameongeza.
Bw Sasse, ni mwanachama mhafidhina katika chama cha Republican. Bado hajatangaza kuunga mkono mgombea yeyote kati ya wanaopambana na Bw Trump, lakini amepigia debe Marco Rubio na Ted Cruz.
Donald Trump amegawanya wengi hasa kwa matamshi yake ambayo yamekuwa yakizua utata.
Moja ya haya ni pendekezo lake la kujenga ua mpaka wa Mexico na Marekani ili kuzuia wahamiaji kuingia Marekani.
Aidha, mwishoni mwa mwaka uliopita, alipendekeza Waislamu wazuiwe kuingia nchini Marekani.

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AZINDUA MRADI WA MAJI MKOANI KILIMANJARO


Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge amezindua mradi wa maji wa Longuo, katika Kijiji cha Longuo, Wilaya ya Moshi mwishoni mwa wiki katika ziara yake mkoani Kilimanjaro. Mradi huo unaohudumia vijiji vya Longuo na Kariwa, umekuwa faraja kubwa kwa wananchi, ambao kwa muda mrefu walikuwa na tatizo la kupata huduma ya majisafi na salama na kusababisha hatari ya magonjwa ya milipuko kwa wananchi.

Mhe. Lwenge, amefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua siku themanini tu kukamilika, na kuipongeza Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Moshi (MUWSA) kwa usimamizi mzuri wa mradi huo. Pia, alitembelea chanzo cha maji, chemchemi ya Kisimeni iliyopo Kata ya Uru Kusini ambayo inachangia uzalishaji wa maji katika Wilaya ya Moshi.

Vilevile, Mhe. Lwenge alitembelea miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA). Katika ziara yake hiyo mkoani Arusha, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, aliweza kufika kwenye chanzo cha maji cha Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji cha Bangata, kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru ambao unachangia asilimia ishirini ya uzalishaji maji kwa Jiji la Arusha. 

Pia, alifika kwenye chanzo cha maji cha chemchemi ya Machare, iliyopo Kata ya Moshono, Wilayani Arumeru iliyovamiwa na wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu kinyume na sheria na kuhatarisha uzalishaji wa maji ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia mji wa Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akizungumza mbele ya Waziri wa Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, viongozi na wananchi wa Longuo, Wilayani Moshi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akimtwika maji mama katika Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi mara baada ya kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.
Jiwe la msingi likiashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga (kulia) na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na viongozi na wataalamu aliombatana nao kwenye ziara yake kwenye chanzo cha maji cha Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji cha Bangata, kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA), Inj. Ruth Koya akimuonyesha Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge moja ya miradi ya maji inayotekelezwa na mamlaka hiyo, Kata ya Moshono, Wilayani Arumeru

Kiwanda cha A to Z Arusha chatozwa faini


Kufuatia kukiuka  sheria za utunzaji mazingira katika  sehemu za kazi Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na  mazingira Luhaga Mpina amekipa siku saba  kiwanda cha A to Z kilichopo  mkoani  Arusha kulipa adhabu ya faini ya shilingi million sabini,na kuongeza kuwa kutokulipwa kwa gharama hiyo kutasababisha kiwanda hicho kufungwa.
Akiwa jijini Arusha Naibu Waziri ofisi ya makamu ya rais muungano na mazingira ametembelea  soko kuu  pamoja na eneo la machinjio  na baadae kuelekea katika maeneo ya viwanda .
Akiwa katika kiwanda cha kutengeneza nguo na bidhaa za plastiki cha A to Z Naibu Waziri  aliyeambatana na wataalamu wa mazingira wamefanya ukaguzi  katika kiwanda hicho na baadae katika maelezo yake ndipo ilipobainika kuwa kiwanda kilipewa adhabu ya kulipa shilingi million sabini iliyotolewa mwishoni mwa mwaka jana  kwa ni kosa  la kukiuka sheria ya mazingira ambayo mpaka hivi sasa haijatekelezwa.
Safari haikuishia hapo bali ikaendelea hadi katika kiwanda cha SAN FLAG pamoja na kiwanda cha  chuma cha Lodhia ambapo Naibu Waziri amewataka wataalamu kutoka baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira kutoa tathmini za namna gani shughuli za uzalishaji unaharibu mazingira kiwandani hapo.
Kwa upande wao viongozi wa viwanda  alivyotembelea Naibu Waziri Luhaga  wameonekana wakijitetea  kwa namna walivyopokea agizo kutoka serikalini hata hivyo msimamo wa serikali haujaweza kubadilika .
Ziara ya naibu waziri imefanyika ikiwa na lengo la kushiriki na wananchi wa Arusha katika kutekeleza siku ya usafi iliyotangazwa na serikali lakini pia ikiwa ni wiki ya usafi barani Afrika.

Kikwete: Nitaachia Uenyekiti wa CCM, Lakini Sitaacha Vikao vya Ndani CCM





Moja kati ya hoja zinazogonga vichwa vya baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mabadiliko ya Uenyekiti wa Chama hicho ambayo yatamuwezesha mzee wa Kutumbua Majipu, Rais John Magufuli kuanzisha operesheni hiyo ndani ya chama hicho.

Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete amesema kuwa ataachia nafasi hiyo hivi karibuni na kumkabidhi Rais Magufuli, lakini alitoa angalizo kuhusu uhusika wake kwenye chama hicho baada ya kujivua kofia hiyo nzito.

Ingawa Katiba ya Chama hicho inaeleza kuwa mwenyekiti mpya atapatikana mwaka 2017, Mwenyekiti wa Chamo hicho, Dk. Jakaya Kikwete amepanga kuachia nafasi hiyo mapema (mwaka huu) kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake.

Akiongea jana kwenye uzinduzi wa Kitabu cha maisha ya kada maarufu wa chama hicho, Marehemu Captain John Komba, Dk. Kikwete alieleza kuwa ataachia nafasi hiyo lakini hataacha kushiriki vikao vya ndani na mambo ya maamuzi ya chama hicho.

“Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi nitaachia, lakini mambo ya ndani yanayohusu chama hiki sitaacha kushiriki,” alisema.

Februari mwaka huu, Dk. Kikwete aliwaambia wazee wa CCM mjini Singida kuwa sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa chama hicho mwaka huu, zilikuwa sherehe zake za mwisho akiwa kama Mwenyekiti.