Monday, June 6, 2016

VANESA MDEE

WATOTO WAKITANZANIA

Samia aagiza kuundwa kamati za mazingira

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameagiza wananchi katika ngazi zote kuunda kamati ndogo za mazingira zitakazosimamia sheria ndogo za mazingira na utunzaji wa misitu ili kulinda na kuokoa vyanzo ya maji.
Amewataka wananchi kwa utashi wao kuhakikisha katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani wanashiriki kikamilifu katika kusimamia na kuhakikisha vyanzo vya maji vinahifadhiwa ili binadamu na wanyamapori waishi.
“Nielekeze kuwa, kamati za mazingira katika ngazi za vijiji, vitongoji, mitaa, kata na wilaya ambazo sheria ya mazingira imeelekeza ziwepo, zianzishwe au zifufuliwe na zichukue nafasi ya kutambua na kusimamia vyanzo vya maji vilivyopo,” alisisitiza Samia.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika duniani kote jana, alisema kazi nyingine ya kamati hizo ndogo ni kuhakikisha pia inafufua vyanzo vya maji vilivyoharibiwa kwa kuvihifadhi kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Katika kuadhimisha siku hiyo nchini kaulimbiu ya Tanzania ni ‘tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa letu’. “Maji ni uhai wa viumbe vyote akiwemo binadamu, wanyamapori, mimea na ni uhai wa uchumi wa taifa.”
Kutokana na ukweli huo, Tanzania imeamua kuwa na kaulimbiu hiyo kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira hususan vyanzo vya maji kutokana na kukithiri kwa shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, ufugaji, uchimbaji wa madini na matumizi ya nishati.
Alisema hali hiyo imesababisha kuwepo na upungufu wa mtitiriko wa maji katika mito mingi nchini takribani kwa kipindi cha miongo mitano iliyopita na baadhi ya mito imebadilika na kuwa ya msimu, kuchafuliwa sana na mingine kukauka.
“Tukiendelea na mwenendo huu wa uharibifu wa vyanzo vya maji, mito yetu mikuu hapa nchini kama vile Rufiji, Pangani, Ruaha na mingineyo inayotegemewa sana kwa uhai na ustawi wa Watanzania wengi, itakauka ndani ya miaka 15 ijayo,” alisisitiza.
Akizungumzia maadhimisho ya siku hiyo duniani, alisema kimataifa yanaadhimishwa nchini Angola yakiwa yamebeba kaulimbiu ‘go wild for life save the environment’ inayokumbusha umuhimu wa kuchukua hatua za makusudi kulinda maisha ya wanyamapori.
Kihistoria siku ya mazingira ilianzia mwaka 1972 wakati Baraza la Umoja wa Mataifa lilipopitisha maamuzi ya kuanzishwa kwake kwenye mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira na Maendeleo Endelevu uliofanyika jijini Stockholm nchini Sweden.

Friday, June 3, 2016

PATA ELIMU KUTOKA KIKUNDI CHA MAISHA YA THAMANI NDANI YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA (AJTC)


Kikundi cha MAISHA YA THAMANI kinacholenga kutoa elimu kwa jamii ya kitanzania inayoratibiwa na Bw Fedinand Shayo, kinatoa elimu ya Maisha kwa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha AJTC.


Mkurugenzi wa Mafunzo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha.Bw Joseph Mayagila 

Mtangazaji wa Redio Five 5, Bw Godfrey Thomas akizungumza na wanafunzi wa AJTC

Wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa habari na utangazaji Arusha,Wakisikiliza mafunzo kutoka kwa wageni wao...MAISHA YA THAMANI


Wakufunzi wa Chuo cha uandishi wa Habari na utangazaji Arusha Bw Andrea ngobole kutoka kushoto,na Mwl Elihuruma Chao ...kulia


Mkufunzi wa AJTC Bw Andrea Ngobole akizungumza na wanafunzi kwenye Semina ya MAISHA YA THAMANI



Bw Proti Profit Manga akitoa elimu ya maisha kwa wanafunzi wa AJTC




Bi Hellen akitoa elimu kwa wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha

Bw Fedinand Shayo Mratibu wa MAISHA YA THAMANI. Picha na PPM



Na RAYMOND WILLIAM

MR&MRS ELIHURUMA CHAO

TUMTEGEMEE MUNGU KWA KILA JAMBO

KIKAO CHA KWANZA CHA BUNGE LA (AJTC) MASWALI NA MAJIBU NDANI YA UKUMBI WA CHUO HICHO


 Kikao cha bunge la wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari kilichowakutanisha baadhi mawaziri
kutoka wizara tofauti tofauti kwa lengo la kuwasilisha ripoti na kujibu maswali ya wabunge hao.
Wizara ambazo zilitakiwa kuwasilisha ripoti zao ni wizara ya Habari,fedha,wizara ya sheria na maadili pamoja na wizara ya afya ulinzi na makazi.Kutokana na wingi wa maswali mengi kwa wizara ya habari  hivyo kupelekea wizara nyingine kutowasilisha ripoti                                                            
 
Spika wa bunge Mh Gabriel(kushoto) akiwa na katibu wa bunge Mh Elizabeth Gabrie


Mh Elia Baraka naibu waziri wa Elimu akijibu maswali yaliyoulizwa na wabunge






Mawaziri na manaibu waziri wa wizara mbalimbali wakisubiri kutumbuliwa na wabunge

Thursday, June 2, 2016

TCRA iungwe mkono kuondoa simu feki


TANGU Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipotoa tamko mwezi Desemba mwaka jana kuwa itazifungia simu feki, yamekuwapo malalamiko ya wananchi na wafanyabiashara, wanaotaka muda huo uongezwe.
Mpaka sasa zimebaki siku 13 tu kwa TCRA kuchukua hatua hiyo huku Watanzania wanaotumia simu hizo wakiwa asilimia 18 kutoka asilimia 40 ya awali, kabla ya tangazo hilo.
Kitu cha kushangaza ni kuwa wengi wanaodai kuongezewa muda ni wafanyabiashara, ambao wanataka wamalize kwanza mzigo wa simu feki walizoingiza kwa kuwauzia Watanzania, ambao hawatakiwi kuwa na simu feki.
Kifungu cha 84 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, kinataka kuwepo kwa mfumo wa Rajisi ya Namba za Utambulisho wa Vifaa vya Mawasiliano vya Mkononi, ambayo inatakiwa ihifadhiwe na kuendeshwa na TCRA.
Pia sheria hiyo inawataka watoa huduma wa mawasiliano, yanayotumia vifaa vya mkononi kuweka mfumo wa kudumu wa kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mkononi, vinavyotumika kwenye mitandao yao.
Kwa maana hiyo, kutakuwa na utambuzi wa kati ya mtumiaji wa simu na kifaa chake kwenye kampuni hizo, hivyo kutoa na fursa ya wananchi kuwa na matumzi sahihi ya simu, ikiwa tofauti na sasa.
Kwa muda sasa kumekuwapo na kilio cha wananchi ya kuibiwa fedha zao kupitia simu au kuibiwa simu zenyewe. Ili kuondokana na tatizo hilo, basi wakati umefika sasa kwa Watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia TCRA ya kuondoa simu feki katika soko la Tanzania kwa manufaa ya wananchi.
Wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa mfumo huu wa kielektroniki wa Rajisi, ambao utahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi, una lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa, kuharibika, kupotea au ambavyo havikidhiviwango vya matumizi katika soko la mawasiliano.
Endapo mtu atapigiwa simu na kutapeliwa fedha, mfumo huo utaweza kutambua namba tambulishi ya simu ambayo imetumika na mtu aliyeisajili. Ni rahisi kufuatilia mtu mwenye simu halisi na ni ngumu kwa mtu mwenye simu feki.
Pia mfumo huo utasaidia kuondoa tatizo la wizi wa simu, kwani mtu aliyeibiwa akitoa taarifa za kupotelewa kwa simu yake, simu hiyo itafungwa ; na ikishafungwa haitaweza kutumika na mtandao wowote wa simu hapa nchini, kwa maana nyingine aliyenunua simu hiyo ya wizi atabaki na ‘toy’ Pia hatua hiyo itahimiza utii wa sheria, kwani Kifungu cha 128 cha EPOCA kinachomtaka mtumiaji wa simu, kutoa taarifa ya kupotea au kuibiwa kwa simu au laini ya simu na Kifungu cha 134 cha Sheria hiyo, kinachotaka kampuni za simu kutotoa huduma kwa simu ambayo imefungiwa, kama ilivyoelezwa hapo juu.
Mteja anapopoteza tu simu yake ya kiganjani, anatakiwa kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha karibu, ambapo atapewa namba ya kumbukumbu ya taarifa ya tukio, maarufu kama RB na kuipeleka kwa mtoa huduma, ambaye baada ya kuhakiki, ataifungia simu hiyo isitumike kwenye mitandao mingine ya simu.
Hivyo Mfumo wa Rajisi ya Namba za Utambulisho wa Vifaa vya Mawasiliano vya Mkononi, una lengo la kuwahakikishia watumiaji usalama wakati wanapotumia vifaa hivyo vya mawasiliano, vikiwemo simu za kiganjani na vifaa vya mawasiliano vya kiganjani (tabuleti). Ni vyema watumiaji wa simu na vifaa vingine vya mawasiliano, kuunga mkono juhudi hizo kukomesha tatizo ili kuimarisha usalama wetu.

Tuesday, May 31, 2016

VIJANA NCHINI WASHAURIWA KUJIUNGA NA MASHIRIKA YA KUJITOLEA ILI WAJIONGEZEE UJUZI NA MAARIFA

1
Vijana nchini Tanzania wameshauriwa kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea ili kujiongezea ujuzi, uwezo, maarifa na kuleta mabadiliko katika jamii zao,hayo yalielezwa na Meneja wa Maendeleo ya Vijana wa shirika la Raleigh Tanzania, Genos Martin wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.
Martin alisema kuwa ni vyema kwa vijana kujiunga na mashirika ya kitaifa na ya kimataifa ya kujitolea kwani kwa kufanya hivyo kutawapa vijana fursa ya kuongeza ujuzi na maarifa ambao utawasaidia katika sehemu mbalimbali.
Martin alisema, “Kufanya kazi kwa kujitolea ni kitu kigeni nchini kwetu tofauti na Mataifa ya nchi zilizoendelea, watu waliowahi jitolea wanapewa kipaumbele kwenye maombi ya kazi tofauti na nchini kwetu. Hii inafanya kujitolea kuwa jambo la muhimu sana kwenye mataifa ya wenzetu” 
 “Vijana wengi wanalalamika kuwa nafasi nyingi za kazi zinawataka wawe na uzoefu wa miaka mitatu nakuendelea, hawajui ni vipi wanaweza kupata uzoefu lakini kama wakijiunga na haya mashirika ya kujitolea wanaweza pata huo uzoefu na kuwafanya wawe na nafasi nzuri pindi waombapo ajira” aliongezea Martin.
Aidha, Afisa Mawasiliano wa Raleigh Tanzania, Kennedy Mmari alieleza kuwa ni kawaida ya shirika hilo kutafuta vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao huungana na vijana wenzao kutoka mataifa ya mbali mbali ya Ulaya na Amerika.
Mmari aliongezea, “Raleigh tuna programu kwa vijana zinazohusu ujasiriamali, usafi, maji na utunzaji wa mazingira, kijana yeyote anaweza kujjiunga nasi na kufanya program zetu. Hatutoi malipo yoyote wala hawatulipi chochote isipokuwa tunagharamia mahitaji yao yote ya msingi pindi wakiwa kwenye programu”
2
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chibe iliyopo kata ya Old Shinyanga mkoani Shinyanga wakishuhudia ufunguzi wa kituo cha elimu ya awali kilichojengwa na na vijana wa kujitolea kwa msaada wa shirika la Raleigh Tanzania.
Kwa upande wa vijana waliofanya programu na shirika hilo  wameshukuru kwa nafasi waliyopewa kwani imewasaidia kupata ujuzi na ufahamu wa mambo tofauti ikiwemo jinsi ya kuandaa na kusiammia biashara.
Mmoja wa vijana ambao wamepata fursa hiyo, Sia Malamsha,  alisema kuwa anajiona wa tofauti baada ya kumaliza programu, hakuwahi fikiria kama kuna watu Tanznaia hawana huduma za maji safi na salama lakini kupitia programu za Raleigh nimeweza fika kwenye jamii hizo na kuwasaidia kutatua matatizo hayo.
“Nimekuwa sehemu ya mabadiliko makubwa katika nchi yangu, najivunia kuona nimefanya kitu kuikomboa jamii ya Watanzania” aliongezea Bi. Malamsha.
3
Vijana wa Shirika la kujitolea la Raleigh wakishiriki ujenzi wa choo katika moja ya miradi yao
Naye kijana Ashiru Said aliyefanya programu ya ujasiriamali amesema kua programu za Raleigh zimemsaidia kupata elimu ya kusimamia na kuendesha biashara.
“Nimeweza kupata elimu ya ujasiriamali, baada ya kurudi nyumbani jamii imefaidika na elimu niliyoipata kwani nimeweza waelimisha vijana wenzangu jinsi ya kuanzisha na kusimamia biashara zao wenyewe” alimalizia Said.
Raleigh Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali lenye ofisi zake mkoani Morogoro na kufanya programu za kujitolea kwa lengo  la kuisaidia jamii ya Tanzania sehemu mbalimbali.(P.T)

Monday, May 30, 2016

MISS TANZANIA USA AEESHA KAMARA ATEMBELEA, KUONGEA NA KUTOA MSAADA KENTON HIGH SCHOOL


Published in Jamii
Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara akiongea na wanafunzi wa Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam siku alipotembelea shuleni hapo katika moja ya majukumu yake ya kuhudumia jumuiya. Miss Kamara anadhamini wanafunzi wawili shuleni hapo
Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akimkabidhi msaada mwalimu mipira siku alipotembela shule ya Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania USA Aesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wawili anaowadhamini kwa kuwasomesha shuleni hapo.
Picha ya pamoja. (P.T)

Friday, May 27, 2016

HATIMAYE MAHIRI WA BONANZA LA UTANGAZAJI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI (AJTC) WAMEPATIKANA



Darasa la Mbuga ya Ngorongoro katika chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha(Ajtc) wakishangilia mara baada
ya kuibuka washindi katika michuano ya utangazaji iliyofanyika chuoni hapo.

Michuano ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaza Arusha
 (A.J.T.C) imemalizika hii leo ambapo mshindi wa kwanza hadi wa mwisho amejulikana.

Darasa lililoibuka kidedea katika mashindano hayo yaliyochukua takribani siku tano linatambulika kwa jina la Mbuga ya Ngorongorongoro.

Mashindano hayo yaliyohusisha madasa 13, darasa la Ngorongoro limejishindia kombe lenye thamani ya Tsh 10,000 pamoja na pesa taslimu Tsh 150,000.
Nafasi ya pili katika michuano hiyo Utangazaji ilichukuliwa na darasa linaloitwa Mlima Kilimanjaro huku wakijinyakulia Tsh10,000 na darasa la Serengeti limeshikilia nafsi ya tatu na kupewa zawadi fedha taslimu Tsh 75,000.
Mkurugenzi wa chuo hicho cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha bw Joseph Mayagila amewapongeza wanafunzi wote walioshiriki na kuwataka waendelee kujituma katika masomo yao ili wafanye vizuri katika tasnia ya uandishi wa habari na utangazaji.

Thursday, May 26, 2016

MASHINDANO YA 9 NDANI YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA (AJTC) YAMEINGIA LEO KWENYE FAINALI YA KUPATA MADARASA MATATU YALIO BORA KATIKA UTANGAZAJI


Papaa Reymond Blessing




Makamu mkuu wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha Bw Elifuraha Samboto (Kushoto) akitoa hotuba fupi kabla ya kuanza fainali ya mashindano yanayoendelea chuoni hapo kutafuta madarasa matatu bora.



Wanafunzi wa AJTC wakiwa kwenye Ukumbi wa Chuo hicho wakisikiliza vipindi kutoka studio za 96.6 AJT FM  PICHA NA SAMWELY WILSON



Majaji wa mashindano ya Utangazaji AJTC Steven Mulaki (kulia),Amos Ishengoma ( Katikati) na Jackline Joel (Kushoto) PICHA NA SAMWELY WILSON(NA Raymond William)

Monday, May 23, 2016

DARASA GANI MAHIRI KWA UTANGAZAJI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA KWA MWAKA 2016


Mashindano ya Utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha katika mwaka  2016 yameanza rasmi siku ya leo.Mashindano hayo ni ya 9 tangu kuanzishwa kwa chuo hichi cha utangazaji.Takribani madarasa 13 yatashiriki na leo yameanza madarasa 3.Madarasa hayo ni pamoja na darasa la Selous,Mt. Evarest na darasa la Mt. Meru na mashindano haya ni maalumu kwa wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho na lengo kuu la mashindano hayo ni kujifunza na  kuwanoa wanafunzi hao ili wanapomaliza chuo wawe na uzoefu wa utangazaji

Mashindano hayo yanatarajia kufikia tamati siku ya Ijumaa ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia Kombe lenye thamani ya sh. 100,000/= na pesa taslimu sh. 150,000/= ,Mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa sh. 100,000/= na mshindi wa tatu atapata pesa Sh. 75,000/=
Kesho mashindano yataendelea kwa madarasa yafuatayo;

Darasa la Mt. Udzungwa, kisha darasa la Serengeti na kumaliziwa na darasa la Aicc
Makamo mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Elifuraha Samboto akifungua rasmi mashindano ya utangazaji katika chuo hicho ambaye pia ni mshauri mkuu wa kamati ya utangazaji chuoni hapo.

Bw. Elifuraha Samboto akitoa maneno mafupi kabla ya ufunguzi wa mashindano ya utangazaji




Mkuu wa kitengo cha utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Onesmo Mbise akitoa maelekezo kwa wanafunzi jinsi ya kutumia vifaa vya utangazaji kabla ya mashindano kuanza



Mwanafunzi wa darasa la Mt. Meru Theobad Jacob akijaribu vifaa vya utangazaji kabla ya mashindano kuanza

Friday, May 20, 2016

MASHINDANO YA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI AJTC JIJINI ARUSHA KUANZA RASMI Tarehe 23/05/2016

Mkufunzi wa AJTC Bw Andrea Ngobole ndani ya studio za 96.6 AJTC FM

ELIHURUMA CHAO Mkufunzi wa Maswala ya Production na Fundi Mitambo wa AJTC Radio akiwa Katika studio za Radio kuhakikisha Mitambo Inakaa sawa


Makamu Mkuu wa chuo cha Uandishi Wa habari na Utangazaji Arusha Bw. ELIFURAHA SAMBOTO Akiwasilisha Taarifa ya Habari

JACKLINE JOELI Mkufunzi wa Arusha Journalism Akiwa katika kipindi cha GOSPEL TIME Cha 96.6 AJTC RADIO

ONESMO ELIA MBISE kulia Mkufunzi wa Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha pia ni Mkuu wakitengo Cha utangazaji Chuoni hapo akiwa katika kipindi cha ELIMIKA NAMI

Pichani Ni STEPHEN MULAKI Katika Makala Murua ya DUNIA Makala inayohusiana na Watu wenye Ulemavu wa ngozi ALBINO

Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa habari nautangazaji Arusha wakiwa makini kuwasikiliza wakufunzi wao
Mashindano hayo yataanza Rasmi jumatatu ijayo ya  Tarehe 23/05/2016  hadi tarehe 27/05/2016 siku ya ijumaa

HII NI KAWAIDA NA NI DESTURI YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA (A..J.T.C) KILICHOPO ARUSHA MBAUDA KWA MROMBO KUANDAA MASHINDANO YA UTANGAZAJI KILA WAKATI KUWAPA UWEZO WANAFUNZI KUPAMBANA NA SOKO LA AJIRA PINDI WANAPOMALIZA CHUO