Showing posts with label HABARI ZA MICHEZO KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label HABARI ZA MICHEZO KIMATAIFA. Show all posts

Wednesday, March 2, 2016

Leicester City washindwa kutamba EPL


Salomon RondonImage copyrightGettyImage captionRondon alitangulia kufunga dakika ya 11
Leicester wamepoteza nafasi ya kufungua mwanya wa alama tano kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kutoka sare 2-2 na West Brom.
Salomon Rondon alimkwepa Robert Huth na kuwapa West Brom uongozi dakika ya 11 lakini Danny Drinkwater alisawazishia Leicester.
Andy King aliwaweka Leicester uongozini lakini Craig Gardner alisawazishia West Brom kupitia mkwaju wa adhabu.
Leicester waligonga mwamba mara mbili katika mechi hiyo iliyochezewa uwanja wao wa nyumbani wa King Power Stadium, lakini hawakubahatika kupata bao la ushindi.
Sare hiyo imewaacha Leicester alama tatu pekee mbele ya Tottenham Hostspur.
Spurs wanaweza kwenda kileleni iwapo watafanikiwa kuwashinda West Ham uwanjani Upton Park Jumatano.
Leciester wamo alama sita mbele ya Arsenal ambao watakutana na Swansea Jumatano.
West Brom, ambao sasa wameshindwa mechi mbili pekee kati ya 10 walizocheza majuzi zaidi ligini wamo nambari 13 ligini, alama 12 kutoka eneo la kushushwa ngazi.
Matokeo ya mechi za EPL zilizochezwa Jumanne
  • Aston Villa 1-3 Everton
  • Bournemouth 2-0 Southampton
  • Leicester 2-2 West Brom
  • Norwich 1-2 Chelsea
  • Sunderland 2-2 Crystal Palace

Sunday, February 21, 2016

CHELSEA WAPEWA EVERTON, WATFORD WAINGOJA ARSENAL FA



ArsenalA
Image captionArsenal walitoka sare na Hull City

Chelsea watacheza dhidi ya wapinzani wao katika Ligi ya Premia Everton kwenye robofainali Kombe la FA.
Mshindi kati ya Manchester United na klabu ya Shrewsbury inayocheza ligi ya daraja la tatu Jumatatu atacheza nyumbani dhidi ya West Ham.


Droo hiyo ya robofainali ilifanywa uwanjani Stamford Bridge Jumapili.
Kwingineko Reading, wanaocheza ligi ya daraja la pili, watacheza dhidi ya Crystal Palace nyumbani, nao Watford wawe wageni wa mshindi kati ya Arsenal na Hull mechi ya marudiano.
Arsenal na Hull walikosa kufungana mechi ya raundi ya tano iliyochezwa Jumamosi.
Mechi za nusufainali zitachezwa wikendi ya 11-14 Machi.
Chelsea walilaza Everton katika fainali ya Kombe la FA mwaka 2009 meneja wa sasa wa Chelsea Guus Hiddink alipokuwa kwenye muhula wake wa kwanza kwenye usukali Stamford Bridge.

ChelseaImage copyrightAP
Image captionChelsea walilaza Manchester City 5-1

"Ni zamani sana. Najua wanataka sana kulipiza kisasi. Tunatumai tutaendeleza ufanisi ambao tumekuwa nao Kombe la FA,” alisema Mholanzi huyo baada ya timu yake kulaza Manchester City 5-1 mechi ya raundi ya tano Jumapili.
Matokeo ya mechi za raundi hiyo ambazo tayari zimechezwa ni kama ifuatavyo:
  • Arsenal 0-0 Hull
  • Reading 3-1 West Brom
  • Watford 1-0 Leeds
  • Bournemouth 0-2 Everton
  • Blackburn 1-5 West Ham
  • Tottenham 0-1 Crystal Palace
  • Chelsea 5-1 Manchester City