Wednesday, March 9, 2016

WANDISHI WA HABARI WA ZANZIBAR WATAKIWA KUELIMISHA JAMII JUU YA MARADHI YA KIPINDUPINDU


Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Maafa Zanzibar ndugu Ali Juma Hamad akifungua mafunzo ya waandishi wa habari juu ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu katika Ukumbi wa gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar, (kulia) daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt Fadhili Mohd na (kushoto) Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  
Washiriki wa
  mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhili Mohamed alipokuwa akielezea njia za kukabiliana na kipindupindu katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika Ukumbi wa Gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji Mkame akiwasilisha mada ya wajibu wa waandishi wa habari katika kukabiliana na maradhi ya milipuko katika mafunzo yaliyofanyika Ukumbi wa Gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar.
Katibu wa Jumuiya ya Maafisa wa Afya Zanzibar Ahmed Suleiman Said akitoa elimu ya kupambana na maradhi ya kipindupindu kwa wananchi wa shehia ya Shaurimoyo Mjini Zanzibar.

Baadhi ya wananchi wa shehia ya Shaurimoyo Mjini Zanzibar wakifuatilia juu ya elimu ya ugonjwa wa Kipindupindu iliyotolewa na Jumuiya ya Maafisa wa Afya Zanzibar.

Daktari dhamana kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohammed Abdallah amewataka wananchi kuchukua tahadhari kuhusu maradhi ya kipindupindu ambayo kwa sasa ni tishio kubwa Zanzibar.

Hayo ameyasema katika Ukumbi wa Gereji ya Wizara ya Afya Mombasa kwenye mafunzo ya waandishi wa habari juu ya kujikinga na ugonjwa huo ambao bado unaendelea katika sehemu mbali mbali Zanzibar.

Amesisitiza kuchukuliwa tahadhari zaidi kupambana na maradhi ya kipindu pindu ikiwemo kuweka mazingira safi, kufuata masharti ya afya, kuchemsha maji ya kunywa ama kutumia maji yaliyotiwa dawa ya kuulia bektiria wanaosababisha maradhi hayo..

Dkt. Fadhil amewataka wananchi kuacha tabia ya kula ovyo njiani, kukosha matunda na mboga mboga kabla ya kula na kuchukua tahadhari kubwa wakati wa kumshughulikia maiti ya maradhi ya kipindu pindu kwani ni miongoni mwa njia za maambukizi ya maradhi hayo.

Amewataka waandishi wa habari kutekeleza majuku yao ya kutoa elimu kwa wananchi ili wapate uelewa mkubwa zaidi kukabiliana na maradhi hayo.

Amesema maradhi ya kipindu pindu ingawa ni tishio kwa maisha ya wananchi lakini ni rahisi zaidi kuyadhibiti kuliko maradhi mengine iwapo wananchi watafuata masharti ya afya.

“Waandishi wa habari mnao mchango mkubwa wa kutoa elimu kwa jamii katika kukabiliana na maradhi ya kipindupindu hivyo tunategemea mashirikiano makubwa kutoka kwenu,” alisisitiza Dkt. Fadhili

Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Maafa Zanzibar ndugu Ali Juma Hamad amesema juhudi za pamoja zinahitajika katika kukabiliana na kipindupindu na mchango wa kila mtu na taasisi unahitajika.

Amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kukabiliana na maradhi hayo tokea yalipogundulika mwezi Septemba mwaka jana ikiwa ni kipindi cha jua kali, kuchukua muda mrefu na kusambaa sehemu mbali mbali za Unguja na Pemba kinyume na watu walivyozoea vipindi vya nyuma.

Akiwasilisha mada ya majukumu ya vyombo vya Habari katika kudhibiti miripuko ya maradhi ya kuambukiza, Mkurugenzi wa Idara y Habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji Makame amesema vyombo hiyo vinajukumu la lazima katika kusaidia umma kudhibiti vifo na athari nyengine za kiuchumi na kijamii zinazosababishwa na miripuko ya maradhi .

Katika kufanikisha majukumu hayo Mkurugenzi Rafii ametaka kuongezwa ushirikiano kati ya vyombo vya habari na sekta ya afya ili kupata taarifa sahihi kwa wakati katika kufikisha ujumbe kwa umma.

Aidha amesema utoaji wa elimu ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza kupitia vyombo vya habari liwe suala endelevu ili jamii iweze kupata uwelewa na kubadilika kitabia.

Jumla ya kambi 18 zilifunguliwa na kuhudumia wagonjwa 1066 Unguja na Pemba na kati yao wagonjwa 22 walifariki. Hivi sasa kuna kambi nne tu zinazoendelea kupokea wagonjwa katika kisiwa cha Unguja.

Wakati huo huo Katibu wa Jumuiya ya maafisa wa afya Zanzibar Ahmed Suleiman Saidi amewashauri wananchi wa shehia ya Shaurimoyo kubadili tabia na kuweka mazingira wanayoishi katika hali ya usafi ili kujikinga na kipindupindu.

Alitoa ushauri huo alipokuwa akizungumza na wananchi wa shehia hiyo katika skuli ya Shaurimoyo walipowatembelea kutoa taaluma juu yamaradhi hayo kwa vile shehia hiyo ni miongozi kati ya shehia zilizoathirika na kipindupindu.

RAIS WA VIETNAM, MHE. TRUONG TAN SANG AWASILI TANZANIA

Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe wakiwapungia mkono viongozi mbalimbali waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe wakishuka kutoka kwenye ndege mara walipowasili katika Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akimkaribisha Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (katikati) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere akiongozana na mkewe 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akiwasalimia baadhi ya Watanzania na Wavietnam waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akiangalia vikundi vya ngoma vikivyotumbuiza uwanjani mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. 
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang akiwapungia mkono wacheza ngoma na matarumbeta waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo)

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki wakati wa kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 08 Maachi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda wakiteta jambo wakati wa kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 08 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Halotel wakiwa tayari kumpokea Rais wao wa Vietnam Mhe. Truong Tan Sang akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara yake ya siku tatu.





Vikundi vya burudani ya matarumbeta na ngoma vikitumbuiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam wakati wa kumpokea Rais wa Vietnam aliyewasili nchini kwa ajili ya ziara ya siku tatu akiwa amefuatana na ujumbe wake.

Ndege iliyombeba Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Ndege iliyombeba Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang ikiwa imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Serikali ya Vietnam na Tanzania wakiwa tayari kumpokea Rais wao Mhe. Truong Tan Sang akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa pili kulia) akielekea kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Philip Mahiga

Tuesday, March 8, 2016

CRDB TAWI LA MLIMANI CITY WASHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA WANAWAKE WENYE AKAUNTI ZA MALKIA.


KATIKA kusherekea siku ya Wanawake duniani Benki ya CRDB tawi la Mlimani City washerekea siku hiyo na wanawake wenye kaunti za MALKIA katika tawi hilosiku hiyo ya wanawake hufanyika Machi 8 kila mwaka.
 Keki na vinjwaji mbalimbali ambayo imeandaliwa na wafanyakazi wanawake wabenki ya CRDB  tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika  Machi 8 kila mwaka.
  
 Mgeni rasmi Anna Jeremiah Kaaya akikata keki pamoja na wateja mbalimbali wabenki ya CRDB  tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam kwaajili ya kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.
Wateja wa Akaunti ya MALKIA katika benki ya CRDB  tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakifungua shampeini katika hafla iliyofanyika katika tawi hilo leo.
Meneja huduma kwa wateja wa benki ya  CRDB tawi la Mlimani City, Catherine Momburi akikabidhi zawadi kwa wateja wanawake wenye akaunti ya MALKIA katika tawi hilo.
Mgeni rasmi Anna Jeremiah Kaaya akimlisha keki meneja uhisiano wa mikopo Martha Ngowi wakati wa kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi kila mwaka. 
Wafanyakazi wa CRDB tawi la Mlimani City, Fatma Tinna na Dorice Temu wakijiandaa kugawa zawadi kwa wateja wenye akaunti za MALKIA kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Wafanyakazi wanawake wa benki ya  CRDB tawi  Mliman City wakiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani.
 
Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pampoja mara baada ya kudhimishi siku ya wanawake dunia katika tawi lao jijini Dar es Salaam.
 

Wednesday, March 2, 2016

SHULE DIRECT YASHIRIKI KILI MARATHON KUSAIDIA WANAFUNZI WASIOSIKIA (VIZIWI) KUJIFUNZA


THURSDAY, MARCH 3, 2016


Mgeni Rasmi Afisa Elimu Manispaa ya Moshi, Bw. Deo Tulo Fundi (pichani kulia) akifafanua jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kompyuta zenye matini ya masomo tisa ya Sekondari (kidato cha kwanza – sita), kompyuta hizo zilitolewa na Shule Direct kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika Shule ya Ufundi Sekondari Moshi. (Kushoto ni Bw. Erasmus Kyara, Mkuu wa Shule ya Ufundi Moshi).
Afisa Elimu wa Elimu ya Mahitaji Maalum Manispaa ya Moshi akitoa neno wakati akishuhudia tukio la makabidhiano ya kompyuta zenye matini za kujifunzia zilizotolewa na Shule Direct kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika Shule ya Ufundi Sekondari Moshi.
Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika Shule ya Ufundi Sekondari Moshi na mwalimu wao Mwl. Raphael Lukumai (aliyekaa kulia) wakifurahia pamoja na baadhi ua wageni waliofika shuleni kwao kukabidhi kompyuta zenye masomo tisa ya Sekondari ndani yake.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya ufundi sekondari Moshi wakielekezana jambo katika mojawapo ya kompyuta walizokabidhiwa na Shule Direct, shuleni kwao,
Aneth Gerana, mtanzania wa kwanza mwenye ulemavu wa kusikia kupata shahada ya Chuo Kikuu, ambaye pia alijitokeza kuunga mkono jitihada za Shule Direct, akiongea na baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika shule ya ufundi sekondari Moshi wakati wa hafla fupi ya kukabidhi kompyuta shuleni hapo.
Aneth Gerana na baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia kutoka shule ya ufundi sekondari Moshi, wakifurahia kompyuta zilizotolewa na Shule Direct ili kuwasaidia wanafunzi hao kujifunza kwa urahisi zaidi.
Faraja Nyalandu, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct na Aneth Gerana wakikimbia mbio za kilometa 21.1 wakati wa mbio za Kili Marathon. Shule Direct walishiriki mbio hizo kwa ajili ya kuchangisha fedha kuwezesha upatikanaji wa kompyuta zenye matini ya masomo tisa ya Sekondari kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika shule za Ufundi Sekondari Moshi na Njombe Sekondari ya viziwi.
Wakiwa wenye nyuso za furaha, Faraja Nyalandu, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct, Aneth Gerana na wengine kutoka Shule Direct na marafiki wa Shule Direct mara baada ya kumalizi mbio za kilometa 21.1 wakati wa Kili Marathon.

Namna bora ya kufundisha wanafunzi wenye ulemavu ni kuwafundisha wakiwa wamechanganyika darasa moja na wanafunzi wasio na ulemavu. Hii inamaanisha kwamba kwa wanafunzi wasiosikia ni muhimu walimu watakaofundisha hilo darasa wawe ni wataalamu wa lugha ya ishara ili waweze kufundisha kwa matamshi na ishara ili kukidhi mahitaji ya wote. Hii ni ngumu kwasababu si walimu wengi wenye utaalamu wa lugha ya ishara. Matokeo yake wale wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia wanaachwa nyuma bila kuelewa na hatimaye kufeli masomo yao.

Shule Direct ilitambua umuhimu wa kutafuta mifumo mingine ya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, kuweza kujifunza. Masomo yakiwa ndani ya Kompyuta ni rahisi kwa mwanafunzi huyo kusoma na kujifunza katika kasi yake na kulingana na uelewa wake.
Hivyo, Shule Direct ikaazimia kushiriki mbio za Kili Marathon 2016 ili kuchangisha fedha kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Moshi Technical na Njombe Shule ya Sekondari ya Viziwi (Shule pekee ya Sekondari ya viziwi Tanzania). Fedha hizo ni kwa ajili ya kuwapatia ‘Content Lab’ kila shule. ‘Content Lab’ inakuwa na kompyuta 20, masomo tisa ya Shule Direct yaliyotengenezwa kwa mujibu wa ‘Syllabus’ ya Tanzania yanayowekwa moja kwa moja kwenye kompyuta hizo kurahisisha upatikana ji bila ‘internet’ na kamusi ya lugha ya ishara ya signwiki.

Tarehe 27 Februari 2016, Mgeni rasmi, Afisa Elimu wa Manispaa ya Moshi Bw. Deo Tulo Fundi akiwa na Afisa Elimu wa Elimu ya Mahitaji maalumu wa Manispaa ya Moshi, Bi. Joyce Sawuo walishuhudia awamu ya kwanza ya utoaji wa vifaa hivyo katika Shule ya Sekondari ya Moshi Tech.

Kabla ya makabidhiano hayo, timu ya ufundi ya Shule Direct iliweza kutoa mafunzo ya namna ya kutumia nyenzo hizo kwa walimu na wanafunzi wa Moshi Technical, hususan wale walimu wanaosimamia wanafunzi wenye ulemavu. 

Wakitoa shukrani zao za dhati wakiongozwa na Mwalimu Mkuu wa Moshi Tech Mwl. Erasmus Kyara na Mwalimu msimamizi wa anayesimamia mafunzo ya wanafunzi wenye ulemavu walielezea furaha yao kupata kompyuta hizo zenye nyenzo za kujifunzia, walisema kwa kipindi kirefu sasa wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia wamekuwa wakiwasindikiza tu wenzao kwa maana matokeo yao huwa hayavuki daraja la nne, wanakumbuka kwa jina, mwanafunzi mmoja tu mwenye ulemavu wa kusikia aliyewahi kupata daraja la tatu katika shule hiyo. 

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia shuleni hapo, mwanafunzi wa kidato cha nne, Raphael, alielezea furaha yake kuwa wanafunzi wenye tatizo kama lake wameweza kupatiwa msaada wa kompyuta zenye masomo zitakazowawezesha kujisomea na kuelewa masomo yao zaidi, alishukuru sana kupata nafasi ya kupata mafunzo ya vitendo ya jinsi kutumia kompyuta hizo, zaidi alishukuru kwa fursa ya pekee ya kukutanishwa na mwanadada Aneth Gerana ambaye aliongozana na timu ya Shule Direct. Aneth ni mtanzania wa kwanza mwenye ulemavu wa kusikia aliyefanikiwa kupata shahada ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, naye ni miongoni mwa wadau waliojitokeza kujiunga na Shule Direct katika zoezi hili kwa kuwashirikisha wanafunzi maisha yake na kuwaasa kuwa wafanye bidii katika masomo yao ili waweze kufaulu katika maisha.

Zoezi la kusaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia la Shule Direct lililopatiwa jina la #KiliShuleThon 2016 lilifanikishwa kwa kiasi kikubwa sana na mchango wa wadau mbali mbali wa elimu na maendeleo waliojitokeza kuchangia, pia zoezi hili liliwezeshwa kwa mchango mkubwa na ushirikiano na waandaaji wa Kili Marathon, Benki ya NMB, Freedom Computers Limited na Lensmark Studios

Leicester City washindwa kutamba EPL


Salomon RondonImage copyrightGettyImage captionRondon alitangulia kufunga dakika ya 11
Leicester wamepoteza nafasi ya kufungua mwanya wa alama tano kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kutoka sare 2-2 na West Brom.
Salomon Rondon alimkwepa Robert Huth na kuwapa West Brom uongozi dakika ya 11 lakini Danny Drinkwater alisawazishia Leicester.
Andy King aliwaweka Leicester uongozini lakini Craig Gardner alisawazishia West Brom kupitia mkwaju wa adhabu.
Leicester waligonga mwamba mara mbili katika mechi hiyo iliyochezewa uwanja wao wa nyumbani wa King Power Stadium, lakini hawakubahatika kupata bao la ushindi.
Sare hiyo imewaacha Leicester alama tatu pekee mbele ya Tottenham Hostspur.
Spurs wanaweza kwenda kileleni iwapo watafanikiwa kuwashinda West Ham uwanjani Upton Park Jumatano.
Leciester wamo alama sita mbele ya Arsenal ambao watakutana na Swansea Jumatano.
West Brom, ambao sasa wameshindwa mechi mbili pekee kati ya 10 walizocheza majuzi zaidi ligini wamo nambari 13 ligini, alama 12 kutoka eneo la kushushwa ngazi.
Matokeo ya mechi za EPL zilizochezwa Jumanne
  • Aston Villa 1-3 Everton
  • Bournemouth 2-0 Southampton
  • Leicester 2-2 West Brom
  • Norwich 1-2 Chelsea
  • Sunderland 2-2 Crystal Palace

Nyama ya mbwa yauzwa Ghana


Image captionMbwa ni rafiki mkubwa wa binadamu.
Mbwa ni rafiki mkubwa wa binadamu.
Hilo linafahamika kote duniani iwe ni Afrika, Ulaya ,Marekani na hata kusini mwa Marekani.
Kwa hali halisia kitoweo cha mbwa ni mwiko katika jamii nyingi barani Afrika,,,lakini sio nchini Ghana !
Mwandishi wa BBC wa idhaa ya kiingereza BBC Africa Akwasi Sarpong alipigwa na butwaa alipokuwa katika pita pita zake nchini Ghana alipokutana na wachuuzi wengi tu wakiuza minofu kwa bei nafuu kandokando mwa barabara za mji wa Kandiga.
Kandiga ni mji mdogo ulioko Kaskazini mwa Ghana.
Kitoweo hicho ambacho ni maarufu Kaskazini mwa Ghana ni kama vile mbuzi wa kuchemshwa ama hata kuku wa kienyeji aliyechemshwa na kuuzwa mitaani na mama ntilie.
Image captionNyama ya mbwa yauzwa Ghana
Akwasi anasema kuwa kichwa chemsha cha mbwa kinagharimu Cedis 14 sawa na dola tatu na senti 60.($ 3.60)
Mkia wa mbwa unauzwa ghali zaidi cedis 15 ($3.80).
Vipande vingine vidogo vidogo vya nyama ya mbwa aliyechemshwa akawa rojo anauzwa kwa cedi moja.
Amini usiamini!
Walipokuja Wachina barani Afrika wakifuata mali ghafi na kujenga mabarabara na reli kutoka taifa moja hadi lingine ndipo ufahamu kuwa mbwa ni kitoweo murua sana huko kwao ukaanza kujulikana.
Je si malimwengu haya !

GAPCO YAWAPA NEEMA WALEMAVU KATIKA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON 2016.


Walemavu wakishangilia kwa pamoja na viongozi wa kampuni ya GAPCO ambao walikuwa ndiyo wadhamini mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizofanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita. 
 Walemavu wakianza kutimua mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Viongozi wa kampuni ya GAPCO wakiwa na Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili toka kushoto) akiwaangalia walemavu wakitimua mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mmoja ya walemavu Vosta Peter (30) kutokea Dar es Salam akiongoza katika mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kila mmoja akionyesha ustadi wa kuendesha baskeli.
Mwanadada Linda Macha (32) ambaye aliweza kuwashinda wenzake katika mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita. 
Mshindi wa mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathon 2016, Vosta Peter (30) akishangilia mara baada ya kumaliza. Mbio hizo za Kilometa 10 zilidhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro
Mshindi wa kwanza kwa mbio za walemavu kilomita 10, Vosta Peter (30) akipokea cheki ya Shilingi Milioni Moja kutoka kwa kampuni ya GAPCO, wanaomkabidhi ni Meya wa Manispaa ya Moshi Raymond Mboya (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Gapco Afrika Mashariki, Macharia Irungu (anayepiga makofi toka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO Tanzania, Vijay Nair. 


Na Cathbert Kajuna - Kilimanjaro. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya GAPCO Afrika Mashariki, Macharia Irungu amewataka wanamichezo kujibidishe kwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri katika mashindano wanayoshiriki. 

Akizungumza mwishoni mwa wiki mjini Kilimanjaro wakati wa Mashindano ya Kilimanjaro Marathoni 2016, ambapo GAPCO ndiyo waliodhamini upande wa Walemavu, alisema kuwa wanamichezo wengi walemavu na hata wasiowalemavu hujisahau sana kufanya mazoezi ya kutosha jambo linalowafanya wengi wao kutoweza kufanikiwa kushinda kwenye mashindano. 

Aliongeza kuwa wao kampuni ya GAPCO waliweza kujitolea kuwasaidia walemavu ili waweze kuonyesha vipaji vyao japo mwanzo waliweza kuwasisitiza wafanye mazoezi na ndiyo maana wameweza kufanya vyema. "Napenda kuwaasa wanamichezo wale walemavu na wasio walemavu, wapende kujitoa kufanya mazoezi ya kutosha maana siri ya ushindi ni mazoezi wala hakuna muujiza unaoweza kukupa ushindi kama haujajitoa kufanya mazoezi ya kutosha," alisema Irungu. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Vijay Nair alisema wamefurahishwa na mahudhurio ya watu wenye ulemavu waliojitoa kushiriki mashindano hayo, na wao hawatawatupa wataendelea kuwa nao bega kwa bega. Bw. Nair aliwaasa walemavu wawe na moyo wa upendo na mshikamano ili waonyeshe mfano bora hata wanapojitokeza kusaidiwa wafaidike kwa pamoja. 

Mashindano ya mbio za Kilimanjaro marathon za 10KM kwa walemavu zilidhaminiwa na GAPCO ambapo shindano lilijumuisha baiskeli za walemavu zenye matairi matatu zenye viwango vya kimataifa wapatao 60 kutoka Dar es Salaam, Arusha, Moshi na Zanzibar.