AFISA USTAWI WA JAMII BW.SHIJA NUMBU |
Kitengo cha ustawi wa jamii Tanzania kimelaani vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinavyofanyika na
jamii mbalimbali hapa nchini.
Rai hiyo
imetolewa na Afisa ustawi wa jamii mkoani Arusha BW.SHIJA NUMBU wakati
akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa jamii nyingi zinajihusisha na vitendo vya
unyanyasaji hasa kwa watoto wa kike.
Bw. shija amesema miongoni mwa vitendo hivyo ni
Ukeketaji,kuozeshwa kwa mtoto wa kike kwa
lazima pamoja na ndoa za utotoni.
Hali hiyo
inampelekea mtoto wa kike kukosa haki yake ya msingi kama vile
Elimu,Malezi,Kusikilizwa,Kutoa maamuzi binafsi na kupoteza utu wa mtu.
Kadhalika
ameitaka jamii kufahamu nafasi ya mtoto wa kike katika taifa na kutambua kuwa ndoa ni maridhiano baina ya
watu wawili hivyo utu wa mtu hauwezi kulinganishwa na hali ya maisha.
Kwa upande
wake mkazi wa sanawari Bi Asha Juma ameiomba serikali kushirikiana na ustawi wa
jamii kupitia mahakama kwa kuweka adhabu na ulinzi wa kutosha kwa jamii
zinazohusika na vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment