Walemavu wakishangilia kwa pamoja na viongozi wa kampuni ya GAPCO ambao walikuwa ndiyo wadhamini mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizofanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Walemavu wakianza kutimua mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Viongozi wa kampuni ya GAPCO wakiwa na Mgeni Rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili toka kushoto) akiwaangalia walemavu wakitimua mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mmoja ya walemavu Vosta Peter (30) kutokea Dar es Salam akiongoza katika mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kila mmoja akionyesha ustadi wa kuendesha baskeli.
Mwanadada Linda Macha (32) ambaye aliweza kuwashinda wenzake katika mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mshindi wa mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathon 2016, Vosta Peter (30) akishangilia mara baada ya kumaliza. Mbio hizo za Kilometa 10 zilidhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro
Mshindi wa kwanza kwa mbio za walemavu kilomita 10, Vosta Peter (30) akipokea cheki ya Shilingi Milioni Moja kutoka kwa kampuni ya GAPCO, wanaomkabidhi ni Meya wa Manispaa ya Moshi Raymond Mboya (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Gapco Afrika Mashariki, Macharia Irungu (anayepiga makofi toka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO Tanzania, Vijay Nair.
Na Cathbert Kajuna - Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya GAPCO Afrika Mashariki, Macharia Irungu amewataka wanamichezo kujibidishe kwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri katika mashindano wanayoshiriki.
Akizungumza mwishoni mwa wiki mjini Kilimanjaro wakati wa Mashindano ya Kilimanjaro Marathoni 2016, ambapo GAPCO ndiyo waliodhamini upande wa Walemavu, alisema kuwa wanamichezo wengi walemavu na hata wasiowalemavu hujisahau sana kufanya mazoezi ya kutosha jambo linalowafanya wengi wao kutoweza kufanikiwa kushinda kwenye mashindano.
Aliongeza kuwa wao kampuni ya GAPCO waliweza kujitolea kuwasaidia walemavu ili waweze kuonyesha vipaji vyao japo mwanzo waliweza kuwasisitiza wafanye mazoezi na ndiyo maana wameweza kufanya vyema. "Napenda kuwaasa wanamichezo wale walemavu na wasio walemavu, wapende kujitoa kufanya mazoezi ya kutosha maana siri ya ushindi ni mazoezi wala hakuna muujiza unaoweza kukupa ushindi kama haujajitoa kufanya mazoezi ya kutosha," alisema Irungu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Vijay Nair alisema wamefurahishwa na mahudhurio ya watu wenye ulemavu waliojitoa kushiriki mashindano hayo, na wao hawatawatupa wataendelea kuwa nao bega kwa bega. Bw. Nair aliwaasa walemavu wawe na moyo wa upendo na mshikamano ili waonyeshe mfano bora hata wanapojitokeza kusaidiwa wafaidike kwa pamoja.
Mashindano ya mbio za Kilimanjaro marathon za 10KM kwa walemavu zilidhaminiwa na GAPCO ambapo shindano lilijumuisha baiskeli za walemavu zenye matairi matatu zenye viwango vya kimataifa wapatao 60 kutoka Dar es Salaam, Arusha, Moshi na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment