KATIKA kusherekea siku ya Wanawake duniani Benki ya CRDB tawi la Mlimani City washerekea siku hiyo na wanawake wenye kaunti za MALKIA katika tawi hilosiku hiyo ya wanawake hufanyika Machi 8 kila mwaka.
Keki na vinjwaji mbalimbali ambayo imeandaliwa na wafanyakazi wanawake wabenki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.
Mgeni rasmi Anna Jeremiah Kaaya akikata keki pamoja na wateja mbalimbali wabenki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam kwaajili ya kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.
Wateja wa Akaunti ya MALKIA katika benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakifungua shampeini katika hafla iliyofanyika katika tawi hilo leo.
Meneja huduma kwa wateja wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Catherine Momburi akikabidhi zawadi kwa wateja wanawake wenye akaunti ya MALKIA katika tawi hilo.
Mgeni rasmi Anna Jeremiah Kaaya akimlisha keki meneja uhisiano wa mikopo Martha Ngowi wakati wa kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi kila mwaka.
Wafanyakazi wa CRDB tawi la Mlimani City, Fatma Tinna na Dorice Temu wakijiandaa kugawa zawadi kwa wateja wenye akaunti za MALKIA kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Wafanyakazi wanawake wa benki ya CRDB tawi Mliman City wakiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pampoja mara baada ya kudhimishi siku ya wanawake dunia katika tawi lao jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment