Mtaaluma mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} Bwana Adson Kagiye akiwasilisha mada inayosema Cash Flow Quadrant katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo. |
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} wameaswa kuweka akiba ili waweze kutumia fursa pindi zinapojitokeza.
Hayo yamesemwa na mtaaluma mkuu wa chuo hicho Bwana Adson Kagiye alipokuwa akiwasilisha mada ya cash flow quadrant katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo.
Aidha Bwana Kagiye amewataka wanafunzi kuwa na tabia ya kuweka akiba pamoja na kuwa na malengo huku akiwashauri kutokubali kutumia zaidi ya asilimia 70 ya kipato chao wanachokuwa wamekipata.
Amesema kuwa ili uweze kufanikiwa katika maisha kila mmoja anapaswa kutenga muda wa kazi muda wa kulala pamoja na muda wa kufanya mambo mengine ya zida.
Kwa upande wake mtoa mada mwingine Bi Jackline Joel ameeleza jinsi uwezo binafsi unavyoweza kuwa ntaji ikiwamo uwezo wa kiakili, nguvu, kiuchumi, pamoja na uwezo wa ubunifu.
Mkufunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha {AJTC} Bi. Jackline Joel akiwasilisha mada inayosema uwezo wako ni mtaji katika semina ya ujasiriamali inayoendelea chuoni hapo |
Semina hii ya ujasiriamali imeanza siku ya jumatatu katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha huku mada mbalimbali zikiwasilishwa na wakufunzi wa chuo hicho na inatarajiwa kumalizika siku ya ijumaa ya wiki hii
No comments:
Post a Comment