Monday, February 22, 2016

KIZZA BESIGYE AKAMATWA UGANDA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda


Besigye
Image captionBesigye alizuiliwa na polisi mara tatu wiki iliyopita
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi.
Watu walioshuhudia wanasema amekamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake.
Amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani tangu Ijumaa wakati polisi walimtuhumu kupanga kujitangazia matokeo.
Wakili wake amethibitisha habari za kukamatwa kwake.
Awali kulikuwa na habari kwamba angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuitisha matokeo rasmi ya kina ya uchaguzi wa urais.
PolisiImage copyrightAFP
Image captionPolisi walivamia ofisi za chama cha FDC Ijumaa wiki iliyopita
Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment