Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi zanzibar Jesha salim jecha |
Wakati chama cha Tanzania Democratic Alliance(TADEA) kikitangaza rasmi kushiriki UchaguziMkuu wa marudio wa Zanzibar, utakaofanyika
Machi 20 mwaka huu, Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar (ZEC) leo itaweka
hadharani majina yote ya wagombea watakaoshiriki uchaguzi huo
.Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar utarudiwa baada ya ule wa Oktoba 25, mwaka
jana kufutwa na ZEC
kutokana na kasoro zilizoibukia demokrasia hiyo
muhimu. Katibu Mwenezi wa TADEA, Rashid Mshenga alithibitisha kushiriki
kwa chama hicho baada ya kumaliza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri,
akisema wamejiridhisha kwamba uchaguzi ndiyo mchakato pekee wa
kidemokrasia wa kupata viongozi halali.“Maamuzi ya mwisho tumekubaliana kushiriki katika uchaguzi wa marudio kwa sababu ndio mchakato na utaratibu pekee wa kidemokrasia wa kuwapata viongozi halali wa kuongoza nchi , baada ya uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana kufutwa,” Mshenga.
amesema, chama hicho kitamsimamisha tena mgombea wake wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Juma Ali Khatib na kitasimamisha wagombea katika baadhi ya majimbo kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani.
.TADEA inaungana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Kijamii (CCK), Sauti ya Umma (SAU) pamoja na Tanzania Labour Party (TLP) kuweka wagombea katika uchaguzi wa marudio huku Chama cha Wananchi (CUF) kupitia mgombea wake wa nafasi ya urais, Maalim Seif Sharif Hamad kikisusia uchaguzi huo.
Kwa upande wake, ZEC kupitia Ofisa Mwandamizi ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, alisema mchakato wa kupokea majina ya vyama vitakavyoshiriki katika uchaguzi huo utakamilika leo ambao ndiyo siku ya mwisho.
“Tutaweka hadharani majina ya wagombea wote wa vyama vya siasa watakaoshiriki katika uchaguzi wa marudio leo baada ya kukamilika mchakato huo ambao unatoa nafasi kwa Tume ya Uchaguzi kuchapisha karatasi za kupiga kura,” alieleza ofisa huyo
No comments:
Post a Comment