Serikali imeombwa kuanzisha utaratibu wa kujenga vituo vya
kulelea watoto yatima nchini ili kuwasaidia watoto hao kuondokana matatizo
mbalimbali yanayowakabili baada ya kufiwa na wazazi wao.
Hayo yamesemwa mwenyekiti wa kituo cha kulelea watoto yatima
cha omuaisha Dr Ramathani mvungi kilichopo eneo la Simba jijini Arusha.
Dr mvungi amesema kuwa serikali imekuwa hailipi kipaumbele
suala la kulea watoto yatima jambo linalosababisa watoto hao kuishi katika
maisha ya dhiki na kujiingiza katika matendo maovu kama vile wizi,kuuza miili yao pamoja na
utumiaji wa madawa ya kulevya.
Hata hivyo mwenyekiti huyo ameongeza kwa kusema kuwa anaiomba
serikali pamoja na mashirika binafsi iachane na utaratibu wa kutoa zawadi kwa
watoto hao katika sikukuu pekee,bali ziwe
zinatolewa siku zote kwani mahitaji ni kila siku.
Naye katibu wa kituo hicho Bw Abas Juma ameipongeza jamii
hususani mtu mmoja mmoja kwani wao ndio wamekuwa wakitoa ushirikiano katika
kuwasaidia watoto hao.
Kituo hicho kimeanzishwa takribani miaka kumi (10) iliyopita
vilevile kinajihusisha kulea watoto wa
kike ambao ndio wamekuwa katika mazingira hatarishi zaidi baada ya kufiwa na
wazazi wao.
No comments:
Post a Comment