Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia) akizungumza na baadhi ya wadau walioshiriki mkutano kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani (wa pili kushoto), ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) akiwa na baadhi ya wadau walihudhuria mkutano kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni, Prof. Japhet Killewo, mhadhiri kutoka MUHAS, Dk, Namala Mkopi, daktari bingwa wa watoto na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Watoto (PAT) na Promise Mwakale, Ofisa Uhusiano katika taasisi ya sikoseli.
Mratibu wa matibabu ya Sikoseli katika kitengo ugonjwa huo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Deogratius Soka (katikati) akibadilishana mawazo na wadau. Kushoto ni Promise Mwakale, Ofisa Uhusiano katika taasisi ya sikoseli na kulia ni Dk, Namala Mkopi, daktari bingwa wa watoto na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Watoto (PAT). Imeelezwa Tanzania ni moja ya nchi yenye inadadi kubwa ya wagonjwa wa sikoseli ikikadiriwa kuwa watoto kati ya 8,000 na 11,000 huzaliwa kila mwaka wakiwa tatizo hilo.
Mmoja wa watu wanaosumbuliwa na tatizo la sikoseli, Hadija Abdallah (20) akitoa ushuhuda wake jinsi anavyoweza kuishi maisha ya kawaida licha ya kugunduliwa na ugonjwa huo akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani (wa pili kushoto), ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) akiwa na baadhi ya wadau walihudhuria mkutano kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Dk. Neema Rusibimayila na Dk Sarah Maongezi mkurugenzi masuala ya afya wa Mfuko wa Wanawake na Maendeleo (WAMA).
Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Benjamin William Mkapa Hiv/Aids Foundation, Hellen Mkondya-Senkoro (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Deloitte, Zahra Nensi huku Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani akiangalia wakati wa hafla hiyo. Imeelezwa ugonjwa wa sikoseli unatibika kirahisi endapo utagundulika mapema katika umri mdogo
No comments:
Post a Comment