Wafanyakazi wa kampuni ya KPMG waliokuja kushangilia wenzao kutoka kushoto ni Asha, Mumtaz,Lilian, Witness, Getrude, patricia, desire na Grace.katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine
Na Krantz Mwantepele
Timu ya mpira wa miguu ya kampuni ya uhasibu ya KPMG ilishiriki michuano ya Awesome Bonanza siku ya Jumamosi tarehe 6-Feb 2016 na kuibuka kinara katika kundi lao lililohusisha timu nyingine za makampuni yanayohusika na uhasibu pia.
Michuano hiyo ambayo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine ilianza siku ya jumamosi tarehe 6 feb 2016 ikifanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Park vilivyopo maeneo ya Mnazi Mmoja zamani kidongo chekundu kwa hatua za Makundi kwa kundi la timu kutoka kampuni za uhasibu.
Katika kundi hilo zilikuwepo timu kutoka kampuni za uhasibu za Deloitte, PWC na Innovex.
Timu ya kampuni ya KPMG iliibuka kinara wa kundi hilo kwa kupata ushindi katika mechi zao zote. KPMG ilipata matokeo yafuatayo: KPMG 3-1 PWC, KPMG 4-1 Deloitte , KPMG 2-1 Innovex. Hivyo kuwafanya wasonge mbele katika micuano hiyo itakayoendelea mwezi huu.
Wafungaji wa magoli ya KPMG walikuwa
Jim Mwasigala (3)
Bakari Mkupe (2)
Frank Mboya (2)
Ahmed Mohammed
Daudi Mbaga
Akiongea baada ya mechi hizo kocha mchezaji wa timu ya KPMG, Hamza Mzee amesema ya kwamba timu kampuni ya KPMG imejiandaa vyema na wana uhakika wa kushinda michuano hiyo kwa kuwa wanajali utamaduni wa kufanya mazoezi kupitia michezo kwa kuwa huboresha Afya kwa ujumla.
|
No comments:
Post a Comment