Wednesday, February 24, 2016

Mchepuko Ambwagia Mtoto Hawala!



Mchepuko (1)Mtoto huyo baada ya kuokolewa na wasamaria wema.
Shekidele, Risasi 
MOROGORO: Mwanamke aliyefahamika kama Mama Gladnes, ambaye ni mchepuko wa mtu aliyefahamika kwa jina la Yusuf, Jumamosi iliyopita alimbwagia mtoto mwanaume huyo baada ya kusitishiwa huduma ya malezi, tukio lililotokea huko Nanenane Tubutu, mjini Morogoro.

Baadhi ya wapangaji wa nyumba anayoishi Yusuf , walisikia zogo likitokea katika chumba cha mwenzao na walipokwenda kuangalia kulikoni, wakabaini uwepo wa mama Gladnes aliyekuja kudai matunzo ya mtoto huyo, lakini mwanaume akimkana kuwa siyo mwanaye maana hafanani naye.
Mchepuko (3)“Kusikia hivyo, mama Gladnes alikuja juu na kwa hasira akatoka nje akisema anarudi kwao Kigoma hivyo hawezi kwenda na mtoto wa mtu, akaenda kumtupa mtoto huyo kwenye kichaka kisha akapanda pikipiki iliyomleta na kutokomea.
“Kwa kuwa tunafahamu eneo hilo lina Mbwa wakali nyakati hizo za usiku, mke wangu na jirani Upendo tuliamua kwenda kumuokota mtoto huyo na kulala naye ambapo muda huu tunajiandaa kumpeleka polisi,” alisema mmoja wa wapangaji hao aliyejitambulisha kama Lukinga.
Mchepuko-(2) Yusuf alikiri kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa mtoto huyo ni wake, lakini alimkataa kwa vile mama Gladnes alikiuka makubaliano yao, ambayo yalikuwa jambo hilo liwe siri isiyojulikana kwa familia yake.
Habari zilizopatikana baadaye zilisema wawili hao walikwenda kituo cha polisi na kukutanishwa katika dawati la jinsia, ambako walikubaliana kuwa mwanaume huyo awe anampatia mzazi mwenzake kiasi cha shilingi elfu sitini kila mwezi, kama matunzo kwa mtoto huyo, jambo ambalo lilikubaliwa na wazazi wote.
Afisa mmoja wa polisi aliyezungumza kwa sharti la kutotaja jina kwa kuwa siyo msemaji, alithibitisha kufikiwa kwa makubaliano hayo na kwamba mwanamke huyo amekubali kumchukua na kuendelea kumlea mwanaye ilimradi tu apewe kiasi hicho cha fedha kilichokubaliwa

No comments:

Post a Comment