Wananchi kijijini Arusha wameulalamikia uongozi kuhusu suala zima la usafi hasa kuwepo kwa
takataka katika mitaa yao.
Hayo yamesemwa na wananchi wa mtaa wa ololovono kata ya
sokoni 1 Bw Macha Molleli na Bi Elizabeth Ngowi wakati wakitoa dukuduku hiyo
kwa serikali.
Wamesema mtaa wao una uchafu mwingi na unaweza kusababisha
magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na homa ya matumbo
.
Pia wananchi hao wameulalamikia uongozi kwa kutoshughulikia
suala la usafi ipasavyo ,hasa mzabuni ambaye amepewa majukumu hayo ya kuchukua na kupeleka takataka katika eneo
husika.
Naye mwenyekiti wa mtaa huo Bw Yelome Wambura amekiri kuwepo
kwa uchafu katika mtaa wake ambapo amesema moja ya sababu ni wananchi kutojali
suala la usafi na kusahau kuwa usafi ni afya.
Pia amelalamikia wananchi kutokuwa na elimu kuhusu utunzaji wa mazingira ambapo baadhi
yao hutupa takataka hasa mifuko ya Rambo katika mitaro ya maji na kupelekea
mitaro kuziba.
Vilevile amelalamikia suala zima la utoaji wa zabuni na kusema zabuni mara nyingi
hutolewa kwa upendeleo na kusababisha
mzabuni kufanya kazi kwa matakwa yake yaani
bila kufuata maelekezo husika.
Mwenyekiti huyo ameiasa serikali kutilia mkazo suala la
usafi kwani usafi ndio nguzo ya afya bora na kuitaka serikali kusambaza vizimba
kila mtaa kwa ajili ya kuweka takataka.
No comments:
Post a Comment