wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakiwa katika mazoezi ya vitendo katika studio ya redio yachuo hicho Picha na juliana saimo,JSN |
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji
Arusha(AJTC)wamehimizwa kujifunza kwa vitendo zaidi ili kukabiliana katika soko
la ajira hapa nchini.
Wito huo umetolewa na mwalimu wa kitengo cha utangazaji
chuoni hapo bw. Onesmo Elia Mbise wakati akitoa maoni kwa wanafunzi walio kuwa
na zamu ya utangazaji.
Aidha amewashauri wanafunzi hao kuwa wabunifu zaidi kwa
kipindi hiki kwakua nafasi za ajira zinalenga zaidi watu wenye ubunifu.
Mmoja wa wanafunzi katika chuo hicho bw.Amani Mmbando ametoa shukrani za dhati kwa kitengo cha utangazji kwani huwasaidia wanafunzi
hao kuwa na uzoefu wa kutosha katika tasnia yao ya uandishi wa habari na
utangazaji.
Pia Mmbado ameomba
kuboreshwa kwa studio za chuo ili kuwa za kisasa zaidi na kuongeza morali ya
kujifunza kwa wanafunzi ambao ni wavivu wa kujifunza kwa vitendo.
No comments:
Post a Comment